Uongozi wa TSJ Wamtembelea Mheshimiwa Balozi wa Tanzania Nchini Japan

Tokyo, 25 Julai 2025: Viongozi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kitanzania nchini Japan (TSJ) wamefanya ziara rasmi katika Ubalozi wa Tanzania uliopo Tokyo kwa ajili ya kujitambulisha kwa Mheshimiwa Balozi Baraka Luvanda na kutoa taarifa ya maendeleo ya jumuiya.
Katika hotuba yake, Mwenyekiti wa TSJ Bw. Kinuma Ndaki alielezea mafanikio ya TSJ hadi kufikia Julai 2025, ikiwa ni pamoja na:
- Ushiriki wa TSJ katika Tanzania Day – Osaka Expo 2025,
- Uundwaji wa tovuti mpya ya TSJ
- Kuboresha mfumo wa usajili wa wanachama, na
- Kuendelea kutoa huduma ya ushauri kwa waombaji wa ufadhili wa masomo wanaotamani kuja kusoma Japan.
Aidha, viongozi wa TSJ waliwasilisha ombi rasmi kwa Mheshimiwa Balozi kuhusu kufanyika kwa TSJ Annual General Meeting (AGM) ya mwaka 2025 katika Ubalozi huo tarehe 30 Desemba 2025. Kwa furaha na moyo wa uzalendo, Mheshimiwa Balozi amelipokea na kukubali ombi hilo, na atakuwa Mgeni Rasmi wa TSJ AGM 2025.
TSJ inamshukuru Mheshimiwa Balozi kwa mapokezi ya kifalme, ushauri wa busara, na kuendelea kuwa mlezi wa karibu wa wanafunzi wa Kitanzania nchini Japan.